Jumamosi 4 Oktoba 2025 - 06:44
Mwanamke katika mantiki ya Uislamu si mfungwa wa matamanio ya wenye tamaa

Hawza / Khatibu wa Ijumaa wa Qom alisema: Sote yatupasa kufahamu kwamba Mwanamke katika Uislamu ana nafasi na jukumu kijamii, kimaadili na kifamilia, na jukumu hilo lazima lilindwe na kuheshimiwa.

Kwa mujibu wa mwandishi wa Shirika la Habari la Hawza, Ayatollah Alireza Aʿrafi katika khutba za Sala ya Ijumaa tarehe 11 Mehr 1404 (sawa na 3 Oktoba 2025) zilizofanyika katika Muswalla ya Quds – Qom Iran, akiashiria Aya isemayo:

يَـٰٓأَیُّهَا ٱلَّذِینَ ءَامَنُواْ ٱتَّقُواْ ٱللَّهَ حَقَّ تُقَاتِهِۦ وَلَا تَمُوتُنَّ إِلَّا وَأَنتُم مُّسلِمُونَ

Enyi mlio amini! Mcheni Mwenyezi Mungu kama ipasavyo kumcha; wala msife ila nanyi ni Waislamu.

alisema: Aya hii inaelezea mambo mawili.

Jambo la kwanza, ni kwamba taqwa ina daraja na viwango. Mwanzo wa taqwa ni kujiepusha na madhambi na kutekeleza wajibu. Njia ya taqwa si kusimama sehemu moja. Sanaa ya mwanadamu ni kupanda ngazi za taqwa na kufikia kilele chake. Ni lazima “haki ya taqwa” ipatikane. Mtazamo lazima uwe kwenye vilele na chemchemi za taqwa.

Mkurugenzi wa Hawza nchini Irani aliendelea: Jambo la pili ni kusisitiza juu ya kuendelea katika taqwa. Kusalia katika njia ya Mwenyezi Mungu ndilo sharti la kupata ufanisi wa kudumu, kwa sababu katika safari ya maisha inawezekana mtu akaanguka na akaacha kuendelea na taqwa.

Akiashiria kumbukumbu ya kufariki kwa Bibi Maʿṣūma (sa) alisema: Bibi Maʿṣūma (sa) ni mwanamke ambaye alitia roho katika mji wa Qom, Iran na ulimwengu mzima, na akawa ni kitovu cha harakati za kielimu na za jihadi. Hii ndiyo nafasi ya mwanamke katika Uislamu: kwamba mwanamke mmoja anakuwa roho ya enei, kiini cha uhai wa Hawza, jihadi na mapinduzi, ni Bibi Maʿṣūma (sa), jambo linaloonesha nafasi tukufu ya mwanamke.

Imamu wa Ijumaa wa Qom aliendelea kusema: Bibi Maʿṣūma (sa) alikuwa ni menye kuhama kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, alihama kwa ajili ya kujiunga na ndugu yake, akafanya safari na hijra, na katika njia hiyo akafa kishahidi; akazikwa Qom — mji wa kihistoria wa elimu, jihadi, maadili na kiroho. Haram yake ni mwanga wa uongofu. Hii ni nafasi ya kielimu na ya msingi kwa mwanamke, na kila mtu anapaswa kupata msukumo kutoka kwake.

Alisema: Mwanamke katika mantiki ya Uislamu si mfungwa wa matamanio ya wenye tamaa, bali yuko kama Bibi Khadīja, Bibi Zahra, Bibi Zaynab na Bibi Maʿṣūma (sa). Hivyo ndivyo ilivyo nafasi, jukumu la kijamii, kimaadili na kifamilia la mwanamke katika Uislamu, na jukumu hilo lazima lilindwe. Wote tunapaswa kuelewa kwamba nafasi hii ya kistaarabu na jukumu hili mahsusi kwa mwanamke limeelezwa na kufufuliwa upya katika Mapinduzi ya Kiislamu.

Khatibu wa Ijumaa Qom, akiadhimisha kumbukumbu ya kuuawa kishahidi Sayyid Ḥasan Naṣrullāh, Sayyid Hāshim Ṣafī al-Dīn na mashahidi wa muqāwama, alisema: Shahidi Sayyid Ḥasan Naṣrallāh alikuwa ni ajabu ya zama hizi, kamanda mkubwa wa muqāwama na nembo ya kusimama imara. Alikuwa ni fahari kubwa kwa ulimwengu mzima wa Kiislamu, mhimili wa muqāwama na heshima kwa Iran.

Aliendelea kusema: Leo hii Iran, eneo la Mashariki ya Kati na ulimwengu wa Kiislamu zipo katika moja ya vipindi vya kihistoria vilivyo nyeti mno; ni nukta ya mabadiliko makubwa katika historia ya dunia, historia ya eneo, historia ya ulimwengu wa Kiislamu na historia ya Iran. Maadui wa Mwenyezi Mungu na mabeberu wa dunia wameanzisha vita vipya vya msalaba, na ukoloni umepita mipaka yote.

Khatibu wa Ijumaa Qom akaendelea kusema: Utawala dhaifu wa Marekani unasema “lazima mjisalimishe” ilhali mfano wa Libya upo dhahiri. Vita vya tamaduni ni nyenzo kwa ajili ya malengo yao ya kimkakati. Wameandaa mazingira ili nguvu mpya isipate kuchipuka katika dunia, Mashariki ya Kati na Asia ya Magharibi, na ili ulimwengu wa Kiislamu usiweze kupumzika, Huu ni msiba mkubwa.

Alisema: Waarabu na Waislamu wanapaswa kujua kwamba ikiwa leo wataghafilika na wasiwe na uwepo sahihi katika uwanja, basi hatima chungu na uharibifu mzito unawasubiri, isipokuwa tu tukifahamu kwa akili, tukasimama pamoja na tukapinga maneno ya kipuuzi.

Mkurugenzi wa Hawza alisema: Wao (maadui) wanasema: “Hampaswi kuwa na makombora, silaha, nguvu ya kujihami, wala siasa na uchumi huru. Mnapaswa kuwa wanyonge na tegemezi kwetu, huenda hapo mkapata faraja ya kiasi fulani.”

Akiashiria ukatili unaofanywa na utawala wa Kizayuni dhidi ya misafara ya Ṣumūd (صمود), alisema: Wao hawashikilii wala kuheshimu hata moja ya thamani ya haki za binadamu ambazo wao wenyewe huzitaja; hawajali vigezo vyovyote vya kibinadamu, na wamekanyaga sheria zote za kibinadamu, za kimungu na za kimataifa. Ghaza ni maonyesho ya ukatili usio na kikomo wa maadui na dhulma isiyo na mwisho ya taifa moja.

Alisisitiza kwamba: Maadui wanapaswa kujua kwamba huenda wakateka baadhi ya ngome, lakini ngome ya mwisho imo mikononi mwa Mwenyezi Mungu na Mujahidina katika njia ya Mwenyezi Mungu. Kwa msaada wa Mwenyezi Mungu, na safu imara za Umma wa Kiislamu zitasimama imara dhidi yao, zitawasukuma nyuma na kuwashinda.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha